Saturday, June 6, 2009

Yesu Aua Wawili na Kujeruhi Saba Kwenye Kliniki ya Utoaji Mimba

Yesu akiwa chini ya ulinzi huku picha ndogo ikionyesha mmoja wa majeruhi akipandishwa kwenye ambulensi.

Jamaa mmoja wa Marekani anayejiita Yesu Kristo amewaua watu wawili na kujeruhi watu saba wakati alipovurumusha risasi kwenye chumba cha wanawake wanaosubiria kutoa mimba zao huku akisema 'Ingekuwaje kama bikira maria angeamua kuitoa mimba yangu, je?

Jamaa huyo anayejiita Yesu Kristu au Massiah akiwa amevalia kama Yesu, aliingia kwenye kliniki ya utoaji mimba ya Huntsville na kuanza kupiga risasi hovyo kwenye chumba cha mapumziko ambacho wanawake wajawazito hukaa humo wakati wakisubiria kutoa mimba zao.

Walinzi katika kliniki hiyo walifanikiwa kumwahi Yesu Massiah kabla hajaikoki tena bunduki yake Glock 9mm aliyoinunua kihalali kwenye duka moja nchini humo.

"Kutoa mimba ni dhambi" alisema Yesu wakati alipokuwa akipelekwa kituo cha polisi baada ya kukamatwa akiwa amefungwa pingu na kuongeza "Ni kitu ambacho siwezi nikakifumbia macho".

Mashuhuda wa tukio hilo walisema kwamba jamaa huyo aliibuka ghafla na kuanza mashambulizi yake ambayo yalipoteza maisha ya Dr. Nelson Woodring, 51, na nesi Danielle Costa, 29.

"Alikuja kwenye meza ya maulizo na kuuliza kama anaweza kumuona Dr. Woodring," alisema mhudumu kwenye meza ya maulizo na kuongeza "Kilichofuatia baada ya hapo alikuwa akisoma mistari ya biblia huku akipiga risasi kwa kila kitu alichokiona".

"Hali ilikuwa inatisha sana" alisema nesi mmoja ambaye alipigwa risasi ya mkononi na tumboni na hivi sasa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu.

"Alimfata Dr. Woodring na kuweka mikono yake kichwani mwake na kumwambia "Nimekusamehe madhambi yako" halafu akampiga risasi kwenye paji la uso".

Maafisa polisi wa Huntsville hawajapata jibu Yesu huyo aliingiaje na silaha kwenye kliniki hiyo pamoja na kwamba kuna ulinzi mkali getini na kukiwa na kamera za ulinzi kila kona.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye selo yake Yesu alisema kwamba hajutii hata kidogo kwa mauaji aliyofanya.

"Kama nilivyosema kwenye John 16:21, maisha ya kila kitu ni ya thamani sana, sio tu kwa wale ambao wameishazaliwa, baba yangu, Mungu anafikiria kama ninavyofikiria".

Yesu aliendelea kusema: " Ingekuwaje kama bikira Maria angeamua kuitoa mimba yangu, ningezaliwa?, inawezekana alifikiria kama hivyo lakini aliamua kutoitoa mimba yake na kunizaa, alifanya jambo sahihi kabisa, kukaa na mimba yake hadi mwisho na kuipatia dunia mkombozi, ni mwanamke aliyebarikiwa sana"

Kwa mujibu wa wataalamu wa sheria, Yesu anaweza akahukumiwa adhabu ya kifo iwapo atapatikana na hatia.

"Kwa jaji sahihi na waendesha mashtaka wazuri Yesu atauliwa tena kwa mara nyingine" alisema profesa wa sheria wa chuo kikuu cha Michigan Profesa Arthur Lipscomb.

Yesu kwa upande wake amesema kuwa haogopi adhabu ya kifo na kusema "Niko tayari kufa kwaajili ya dhambi za wengine".


(kwa hisani ya mwana BIDII Thomas, Aliko)

1 comment:

Anonymous said...

wewe mwana bidii mbona husemi ukweli stori hii umeikopi nifahamishe.com?
Acha hizo wewe wape haki zao nifahamishe badala ya kujipa maujiko tu

GEORGE